Habari za michezo
SIMBA, YANGA ZAIGANA MATOKEO MECHI ZA MAZOEZI….
admin
September 10, 2023
1:23 pm
Wakongwe Yanga na Simba zimegawa dozi nzito kwenye mechi zao za kirafiki baada ya kushinda mabao 6-0 kila mmoja wakiendelea kujipima.
Tuanze na Simba ambao wakicheza kwenye Uwanja wao wa mazoezi pale MO Simba wamejipima dhidi ya Ngome na kufanikiwa kushinda kwa mabao 6-0.
Mabao ya Simba kwenye mchezo huo yamefungwa na mshambuliaji Jean Baleke aliyefunga mara mbili,Aubin Kramo, Willy Onana,Shomari Kapombe na Shaban Idd Chilunda.
Huo unakuwa mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Simba tangu ligi isimame kupisha mechi za Kimataifa kwa Kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ambapo tayari walishazichapa Kipanga (3-0) kisha wakawachapa CosmoPolitan (5-1).
Yanga wakacheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Kiluvya United wakishinda kwa mabao 6-0 mchezo ukipigwa pale Uwanja wao wa mazoezi AVIC Town.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Crispin Ngushi, Farid Mussa huku Hafidh Konkoni, Kennedy Musonda wote wakifunga mara mbili kila mmoja.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.