Habari za michezo

KAZE AFUNGUKA BAADA YA KUANZA MSIMU VIBAYA

Staff Desk September 10, 2023 12:42 pm

Baada ya kuanza vibaya kwenye michezo yao miwili ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa kikosi cha Namungo FC, Cedric Kaze ameweka wazi kuwa tayari wameona wapi walikuwa wanakosea na kuahidi kufanya makubwa kwenye michezo yao ijayo.

Kocha huyo kutoka nchini Burundi ameweka wazi kuwa anajivunia namna ambavyo wachezaji wake wamekuwa wakitimiza maelekezo ya Program anazotoa.

Kaze amesema: Nafurahishwa na namna ambavyo tumekuwa na maendeleo mazuri ya Programu za maandalizi ya michezo yetu ijayo hasa kutokana na kuanza ligi kwa kusuasua.

Tumerekebisha makosa yetu na sasa ni muhimu kuendelea na kasi hii kwa ajili ya mechi zijazo kwani ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo.”

GAMONDI ATAMBA, AWEKA WAZI REKODI YAKE HII MPYA LIGI YA MABIGWA MASTAA SIMBA WACHIMBWA MIKWARA OLE WAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply