Habari za Yanga SC
Habari za michezo

GAMONDI- AL MERRIKH WANAPIGIKA KIRAHISI TU…

admin September 12, 2023 7:23 pm

Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi raia Argentina, amewaangalia wapinzani wake katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Merrikh ya Sudan, kisha akasema hawezi kuwa na presha ya kupata matokeo mazuri mbele yao kutokana na kikosi imara alichoachiwa na mtangulizi wake, Nasreddine Nabi.

Gamondi ametoa kauli hiyo kuelekea mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza dhidi ya AI Merrikh unaotarajiwa kupigwa Septemba 16, mwaka huu nchini Rwanda.

Gamondi amesema anachokiangalia kwa sasa ni kupata matokeo ya ushindi dhidi ya wapinzani wake hao na hana presha yoyote kufanikisha Young Africans kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

β€œKitu kikubwa kwa sasa ni kwamba tunaendelea kujenga timu ili kupata matokeo bora katika mchezo ujao dhidi ya Al Merrikh ya Sudan, tunachokiangalia kwa ukubwa ni ubora wa wapinzani wetu kwa namna walivyo ingawa ninawaamini wachezaji waliopo kwenye kikosi changu.

β€œUnajua suala la uzoefu, sina presha nalo kwa sababu asilimia kubwa ya wachezaji wetu wameshacheza haya mashindano, wanajua nini ambacho tunahitaji ingawa kuna mambo ya kuongeza ili kupata matokeo mazuri zaidi na kusonga mbele, hata ukiangalia msimu uliopita walifanya vizuri sana katika michuano hii,” amesema Gamondi.

SIMBA KUWAFUATA WAZAMBIA KIMAFIA…. BAADA YA KUONA MAMBO MAGUMU…KRAMO AOMBA KURUDI KWAO KUJIPANGA UPYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply