Home Habari za michezo FAILI LA MASTAA HATARI WA EL MERRIKH LATUA KWA GAMONDI….”STAA HUYU ATAWATESA...

FAILI LA MASTAA HATARI WA EL MERRIKH LATUA KWA GAMONDI….”STAA HUYU ATAWATESA SANA”…

Habari za Yanga

YANGA imewafanyia umafia Al Merrikh ya Sudan baada ya kuwanasa mastaa wanane walioiwakilisha timu ya taifa ya Sudan iliyopambana na DR Congo ya Fiston Mayele, watakaounda kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa wikiendi hii, jijini Kigali.

Ipo hivi. Katika kikosi cha Sudan kilichocheza juzi usiku na DR Congo na kufungwa mabao 2-0 jijini Kishansa, kilikuwa na wachezaji wanane wa El Merreikh, huku wengine wakiwa wa Al Hilal iliyowahi kuitibulia Yanga kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Kati ya wachezaji hao, saba walianza kwenye mchezo huo ambao Mayele aliwapiga bao la pili akitokea benchi na kuiwezesha DR Congo kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazofanyika mapema mwakani huko Ivory Coast, huku Kocha Miguel Gamondi akiwafuatilia kupitia kwenye runinga.

Wachezaji hao saba walioanza kwenye mchezo huo, wanne kati yao wanacheza kikosi cha kwanza cha Al Merrikh ikiwa ni panga pangua na huenda wakakutana na Yanga Jumamosi hii, bila kujua kama Gamondi alishawapiga chabo baada ya kugundua janja waliyofanya kabla ya mechi hiyo ya Kigali.

Awali, kocha huyo aliwanasa wachezaji hao ambao wote walicheza mechi mbili dhidi ya Otoho d’Oyo ya Congo Brazzaville, kisha Yanga ikapenyezewa kwenye mechi mbili za kirafiki El Merreikh ilizocheza Kigali ikijiandaa kwa mechi ya Kigali, mastaa hao hawakucheza kabisa huku timu hiyo ikipoteza mechi hizo.

Mastaa hao wa Al Merrikh waliocheza dhidi ya Otoho ni pamoja na kipa namba moja Mohamed Mustafa, beki wa kulia Ramadan Agab, beki wa kushoto Bakhit Khamis na beki wa kati Mohamed Karshoum aliyecheza sambamba na beki wa Al Hilal, Mohamed Ahmed.

Wengine ni mshambuliaji Ahmed Mahmoud na Mohamed Shambaly ambaye alitokea benchi na kati ya mastaa hao walioanza kikosi cha kwanza cha Al Merrikh kinachofundishwa na kocha Osama Nabih ni kipa Mustapha, Agab, Kashroum na Shambaly ambao wana uhakika wa kuivaa Yanga Jumamosi jijini Kigali.

Hata hivyo, habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kwamba Gamondi tayari ana mkanda wa mechi ya Al Merrikh dhidi ya Otoho D’oyo ambao mastaa hao wote walicheza mechi hiyo kwa muda tofauti, pia aliufuatilia mchezo wa DR Congo na Sudan kuwasoma zaidi mastaa hao wanane wa Al Merrikh.

Gamondi amesema “Tunaendelea na maandalizi, kitu muhimu kwetu kwanza ni kujiandaa sisi ndani, tunawasubiria pia wachezaji wetu waliokuwa kwenye timu zao za taifa ili warejee wakiwa salama, mpaka sasa hatuna taarifa mbaya ya yeyote aliyeumia huko, tunaamini watarudi wazima,” alisema na kuongeza;

“Tunazo taarifa za Al Merrikh, baadhi ya mastaa wao wapo kwenye timu ya taifa ya Sudan, tunafahamu hata zile mechi wanazocheza Kigali nyota wao wengi hawapo, tutaendelea kufuatilia taarifa zao muhimu.”

SOMA NA HII  MUSONDA APELEKA SHANGWE JANGWANI, ATHIBITISHA KUWA YEYE NI MWAMBA

1 COMMENT