Habari za michezo

KATIKA HILI LA MASHABIKI YANGA NDIO INAONGOZA, ISHU IKO HIVI

Staff Desk September 22, 2023 3:51 pm

Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka kutoka EATC na EA Radio, Ibra Kasuga amesema kuwa Klabu ya Yanga ndiyo inaongoza kwa kuwaposti mashabiki zake kwenye mitandao yake ya kijamii tofauti na vilabu vingine nchini.

Kasuga amesema hayo mara baada ya Yanga kufanikiwa kuondoka na mashabiki wengi kwenda nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wao wa CAF Champions League na kuibuka na ushindi dhidi ya AL-Merrikh ya Sudan.

“Kuna siku nilikaa hapa nikasema, unajua ukipita kwenye page za mitandao ya kijamii za hivi vilabu ambavyo vina nguvu kubwa Simba, Yanga na Azam Fc, page ambayo inaongoza kuwapost mashabiki wao ni page ya Yanga, hata kutoa shukrani ni page ya Yanga.

“Kwa hiyo naweza nikasema matunda mojawapo ya project yao ya Fans Engagement ni hiki ambacho tunakiona ambacho kwangu mimi ni rekodi kwa sababu sijawahi kuona kitu kama hicho (ikiwa na maana kitendo cha kuondoka na umati mkubwa wa mashabiki kwenda nao nchi jirani kuishabikia timu yao),” amesema Ibra Kasuga.

Ikumbukwe kuwa, juzi Septemba 20, 2023 Yanga iliweka mchezo wao dhidi ya Namungo FC kuwa mchezo maalum kwa ajili ya mashabiki wao ambao wamekuwa bega kwa bega kuisapoti timu yao.

SHAFFIH DAUDA AWACHARUKIA MASHABIKI WA SIMBA, ISHU IKO HIVI KAMATA BONABODA NA ZAWADI NYINGINE KIBAO KUPITIA MERIDIANBET…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply