Kocha Mpya Azam FC
Azam FC

RUNGU LA TFF LATUA AZAM KOCHA AKUTWA NA HILI

Staff Desk September 24, 2023 7:04 pm

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemzuia rasmi Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo, raia wa Senegal kusimama kwenye benchi la ufundi la timu hiyo kutokana na sababu za kutokidhi vigezo ambavyo vinatakiwa.

Dabo ambaye tangu ametua nchini amekuwa akikiongoza kikosi hicho amezuiwa kutokana na Leseni A ya UEFA aliyonayo kutokidhi vigezo vya kanuni za soka la Tanzania ambazo haziruhusu kuwa kocha mkuu wa Ligi Kuu.

Chanzo cha kuaminika kutoka TFF kimesema kuwa, Dabo hatambuliki kama kocha mkuu hivyo kutokana na leseni aliyonayo anaruhusiwa kusimama benchi akiwa msaidizi na viongozi wa Azam tayari wanalijua hilo.

“Mwanzo alikuwa anakaa na kutambulika kama kocha mkuu kwa sababu awali walisema atakwenda kuongeza elimu yake, lakini baada ya kuona kimya na maneno mengi tukaona tufuate kanuni tulizojiwekea,” kilisema chanzo.

HIVI NDIVYO MZIMU WA NABI UNAVYOMTESA GAMONDI MWENYE NAMBA KARUDI YANGA GAMONDI AKUNA KICHWA, KUFUMUA KIKOSI CAF

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply