Home Habari za michezo KAMA ULIKUWA HUJUI….HII HAPA REKODI YA KIBABE ILIYOWEKWA NA GOLI LA JOB...

KAMA ULIKUWA HUJUI….HII HAPA REKODI YA KIBABE ILIYOWEKWA NA GOLI LA JOB NDANI YA YANGA…

Habari za Yanga

DICKSON Job, beki mzawa ndani ya kikosi cha Yanga, amevunja rekodi yake aliyoaindika msimu wa 2022/23 kwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza.

Job msimu wa 2022/23 alikamilisha akiwa ametupia bao moja baada ya kucheza mechi 24 na kukomba dakika 2,025, chini ya Kocha Nasreddine Nabi raia wa Tunisia ambapo Yanga ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Kazi imeanza kwa mara nyingine msimu mpya Yanga ikiwa chini ya Miguel Gamondi raia wa Argentina ambapo Job ameanza balaa lake mapema.

Mchezo wa kwanza Job alifungua akaunti ya kucheka na nyavu dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.

Job kafungua akaunti dakika ya 16, huku akicheza mechi mbili za ligi akikomba dakika 180.

SOMA NA HII  MECHI YA KUFUZU CHAN DHIDI YA UGANDA...SIMBA NA YANGA ZASHINDANA KUTOA MAKIPA NA MABEKI TAIFA STARS...