Home Habari za michezo JANJA JANJA YA MORRISON KWISHA….APIGWA PINI NA WANAJESHI…

JANJA JANJA YA MORRISON KWISHA….APIGWA PINI NA WANAJESHI…

Habari za Michezo

WINGA mwenye vituko vingi ndani na nje ya uwanja aliyewahi kutamba nchini katika klabu za Simba na Yanga, Bernard Morrison ‘BM’ amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mabingwa wa Morocco, FAR Rabat, huku akitakiwa kukaa ndani ya jengo la klabu lililopo katika kambi ya jeshi.

FAR Rabat inamilikiwa na jeshi ikifundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi.

Licha ya winga huyo kuonyesha kiwango bora katika mazoezi ya kupima ubora wake hatua ya kumpa mkataba huo, haikuwa rahisi kutokana na rekodi mbovu juu ya nidhamu, lakini baada ya kikao kizito na mabosi wa klabu hiyo hatimaye juzi Ijumaa wakampa mkataba huo kuitumikia timu hiyo.

Morrison ambaye ni raia wa Ghana, katika miezi hiyo 12 hatakiwi kufanya matukio yoyote ya utovu wa nidhamu na ikijitokeza mkataba wake utasitishwa mara moja na kuondoshwa klabuni.

Licha ya mkataba huo mgumu, lakini Morrison katika mazoezi ya wiki mbili aliyoyafanya na FAR Rabat amewashtua kwa kiwango kikubwa, huku baadhi ya mastaa wa timu hiyo wakishinikiza asajiliwe.

Winga huyo anaweza kuanza kucheza wikiendi hii dhidi ya Raja Athletic ukiwa mchezo mgumu wa kwanza pia kwa Nabi ambaye ameshinda mechi zote tatu za mashindano tangu atue Rabat akitoka kuipa Yanga mataji matatu kwa mpigo ndani ya misimu miwili iliyopita na kuifikisha timu hiyo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

hapa nchini mchezaji huyo alivitumia vigogo Simba na Yanga kwa nyakati tofauti na kubeba navyo ubingwa.a

SOMA NA HII  HII HAPA CV LA KUTISHA LA KOCHA MPYA WA SIMBA....MSHAHARA WAKE NI KUFRU TUPU AISEE...