Home Habari za michezo MWAKA MMOJA TOKA ASEPE YANGA….YACOUBA AANIKA SIRI KIBAO YA AZIZ KI…

MWAKA MMOJA TOKA ASEPE YANGA….YACOUBA AANIKA SIRI KIBAO YA AZIZ KI…

Habari za Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz KI yuko kwenye moto mkali kuliko msimu wa kwanza alipojiunga na timu hiyo kutoka Asec Mimosas, kiasi cha kumuibua nyota wa zamani wa timu hiyo, Yacouba Songne aliyefichua kuwa jamaa huyo amepania makubwa na ndio kwanza kazi imeanza.

Yacouba anayekipiga kwa sasa Arta Solar ya Djibouti, amesema  hashtushwi na kiwango cha Aziz KI anachokionyesha kwa sasa na kwamba ubora huo unatokana na kikao ambacho alikifanya na kiungo huyo kabla ya kuondoka nchini.

Yacouba amesema alilazimika kufanya kikao na Aziz KI akimwambia kwamba bila kujali jina lake anaweza kujikuta anapoteza nafasi ya kuendelea kucheza Tanzania kama atashindwa kuonyesha ubora wake mkubwa alionao.

“Nilipokuwa naondoka hapa niliongea naye nikamwambia mwaka wake wa kwanza hajafanya kitu kile ambacho watu walikuwa wanatarajia alitakiwa msimu huu afanye kweli, mimi namjua Aziz tangu nyumbani ni mchezaji wa kiwango kikubwa sana,” amesema Yacouba aliyeichezea Ihefu msimu uliopita na kuongeza;

“Alihitaji muda kuzoea ligi ya hapa unajua Aziz ni mchezaji mwenye ubora mkubwa wa ufundi na hapa ni tofauti soka la Ivory Coast unatakiwa kutumia sana nguvu, alikuwa anapata wakati mgumu kufanya vizuri walikuwa wanamkamia sana.”

Yacouba alisema baada ya kikao hicho, Aziz KI alipania kuliamsha msimu huu na sasa moto wake umeanza huku akisema bado hajafikia juu ya kile alichonacho.

“Aliniambia msimu huu atawasha moto na kwenye nguvu atahakikisha naye anatumia nguvu, nadhani mnaona sio rahisi kuchukua mpira kwake akiwa ameumiliki,” amesema Yocouba na kuongeza;

“Bado hajafika mwisho, namfahamu vyema, msimu huu akiendelea kupandisha kiwango chake kama hivi atafanya makubwa sana, kitu kizuri naona makocha wake nao wanampa majukumu ambayo anayataka kucheza huru, hili litawasumbua sana wapinzani.”

SOMA NA HII  KUHUSU PITSO NA IBENGE KUHUSISHWA NA YANGA ...UKWELI WA MAMBO HUU HAPA...LOLOTE LINAWEZEKANA...