Home Habari za michezo SIMBA KUWAFUATA WAZAMBIA KIMAFIA….

SIMBA KUWAFUATA WAZAMBIA KIMAFIA….

Habari za Simba

UONGOZI wa Simba, umetangaza kuwafuata wapinzani wao Power Dynamos ya nchini Zambia mapema Alhamisi, huku wakiwa na kikosi chote wakijipanga kupangua hujuma za wapinzani wao ili kuanza vizuri Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Kikosi cha Simba hivi sasa kipo kambini kikiwa kinaendelea na maandalizi ya mchezo huo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kutinga hatua ya makundi.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema msafara wa kikosi chao utawahi kusafiri kuelekea Zambia ukiwa na nyota kamili.

Ally alisema lengo la kuwahi mapema siku mbili kabla ya mchezo huo, ni wachezaji kuzoea mazingira ya nchini hapo sambamba na kuandaa mikakati ya ushindi.

Aliongeza kuwa, mchezo huo ni muhimu kwao kupata ushindi utakaowaongezea hali ya kujiamini kuelekea michezo mingine inayofutia ukiwemo wa nyumbani watakaporudiana jijini Dar es Salaam.

“Tumepanga kuanza vizuri katika mchezo huu wa kwanza wa kimataifa tukiwa ugenini, kwani ushindi huo utawapa presha wapinzani tutakaporudiana jijini Dar es Salaam, lakini utawaongezea hali ya kujiamini wachezaji wetu.

“Hivyo basi tumepanga kuwahi kufika Zambia, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo, tukiwa huko mapema wachezaji watazoea mazingira pamoja na viongozi kupambana kupangua fitina za wapinzani wetu.

“Tunafahamu kila timu inajipanga ipate ushindi nyumbani kwake, hivyo tumejipanga katika hilo kwetu hatutaki kupoteza zaidi tunataka ushindi pekee utakaotuwezesha kusonga mbele kimataifa,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  MUZIKI WA SIMBA, KIKOSI CHAKE KIPO HIVI, YANGA YAMALIZANA NA LITOMBO, NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU