Home Habari za Yanga KISA KUINGIA MAKUNDI AFRIKA….SERIKALI YAIPA MAAGIZO HAYA YANGA SC…

KISA KUINGIA MAKUNDI AFRIKA….SERIKALI YAIPA MAAGIZO HAYA YANGA SC…

Yanga SC

NAIBU Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) amesema haoni sababu ya kikosi cha Yanga jinsi kilivyo kushindwa kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza  baada ya Yanga kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Merrikh, mchezo uliopigwa uwanja wa Azam, Chamazi, Dar es Salaam, Mwana FA amesema amekiangalia vizuri kikosi hicho jinsi kinavyocheza na kukiona kimekamilika kiasi kwamba haoni sababu yoyote ya kukosa kufika robo fainali kama ilivyokuwa kwa Simba msimu uliopita.

Yanga imefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuibuka jumla ya mabao 3-0, mechi ya kwanza wakishinda 2-0, uliopigwa nchi Rwanda ambapo Al Merrikh wakitumia uwanja wa Pele.

“Kwa nilivyowaona wachezaji wa Yanga, sitegemei kuona inashia hatua ya makundi pekee nategemea kufika robo kama ilivyokuwa msimu uliopita kwa Simba, sasa ni muda wa kuendelea kuandaa timu yako kwenye mashindano yajayo,” alisema na aliongeza kuwa

Kufanya vizuri kwa timu hizo ni faida kubwa kwa taifa kuendelea kujipatia sifa na kuongeza faida ya kuendelea kupata uwenyeji ikiwemo kwa sasa tumepata nafasi ya kuandaa AFCON, mwaka 2027,” alisema Mwana FA.

Alisisitiza kuwa sasa ni muda wa kufanya vizuri katika mashindano yaliyopo mbele yao kwa ajili ya kuwaanda wachezaji wazawa kwenda kucheza fainali za AFCON.

“Tukumbuke msimu uliopita Simba iliishia makundi ya Afrika, Yanga kuingia kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho, Serikali tunatamani timu zote zinashiriki michuano ya kimataifa zinafika mbali zaidi,” alisema Naibu Waziri huyo.

Naye Kocha wa Yanga, Miguel Angel Gamondi alisema amefurahishwa na kiwango kizuri kilichoonyeshwa na wachezaji wao na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi

Alisema wachezaji wamecheza vizuri licha ya kutengeneza nafasi za wazi wakafanikiwa kupata moja na kutumia vizuri na kuwapeleka katika hatua ya makundi.

“Sasa ni muda wa kuangalia mechi zilizopo mbele yetu, tunafanya maandalizi hatua kwa hatua mechi kwa mechi, kabla ya kufikiria hatua inayofuata ya michuano ya kimataifa kwa tunaangalia mechi yetu ya mbele ambayo ni ligi,” alisema Kocha huyo.

SOMA NA HII  CV ZA KIPA MPYA WA SIMBA NI HATARI, MBRAZILI ANABALAA HUYU