FT: TZ PRISONS 1-3 SIMBA SC
Habari za michezo

SIMBA WABADILI GIA ANGANI KISA MPIRA HUU

Staff Desk October 6, 2023 10:28 am

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa utarejea ukiwa imara zaidi na mwendo mwingine kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutinga hatua ya makundi.

Ikumbukwe kwamba Simba ilifanikiwa mpango kazi kutinga hatua ya makundi kwa faida ya mabao ya ugenini dhidi ya Power Dynamos kwenye mchezo wa kwanza ubao uliposoma Power Dynamos 2-2 Simba.

Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ilicheza mpira ulipowe jina la pira papatupapatu kutokana na kila mchezaji kushindwa kuwa na utulivu.

Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Simba 1-1 Power Dynamos jumla kuwa ni mabao 3-3.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema kufanikisha malengo ya kutinga hatua ya makundi yalikuwa ni malengo yao kinachofuata ni maandalizi kwenye mechi zinazofuata.

“Kupata nafasi ya kufuzu hatua ya makundi sio jambo dogo unaona tulicheza na timu ambayo ilikuwa na upinzani mkubwa. Power Dynamos sio ya kuibeza ilishawahi kutwaa ubingwa wa Shirikisho Afrika.

“Kuelekea kwenye hatua ya makundi kuna maboresho ambayo yatafanyika kwenye maeneo tofautitofauti ili kuwa na mwendelezo mzuri, katika kupata matokeo mazuri,”.

Oktoba 20 Simba ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly ambao ni wa African Super Leagu.

DROO CAF….. YEYOTE NA AJE TU LEO NDIO LEO DROO YA CAF HAPA SIMBA PALE YANGA…… UPI UTABIRI WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply