Home Habari za michezo ROBERTINHO:- SIMBA TUNACHEZA BILA ‘STREES’….

ROBERTINHO:- SIMBA TUNACHEZA BILA ‘STREES’….

Habari za Simba

KOCHA mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amesema ameridhishwa na jinsi ya timu yake ilivyocheza kwa furaha bila ya ‘Strees’ na kupata ushindi mnono ugenini.

Simba juzi ilifanikiwa kushinda mabao 3-1 ugenini dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo uliopigwa uwanja wa kumbukumbu Sokoine, Mbeya.

Kocha Robertinho alisema ushindi wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya Tanzania Prisons umeonyesha ukubwa na ubora wa timu yao licha ya kufungwa bao la mapema wachezaji hawaku changanyikiwa badala yake walitulia na kucheza katika mipango ile ile aliyokuwa amepanga na huo ndio ukubwa wa timu ya Simba.

“Niwapongeze wachezaji kwa jinsiwalivyocheza soka safi lililotupaushindi mnono na alama tatu muhimu, Mchezo huu umeonyesha daraja la Simba lipo juu, tulifungwa bao la mapema lakini halikututoa mchezoni tulimiliki mpira kama kawaida tukasawazisha na kuongeza.

“Mara zote nasisitiza tunapaswa kucheza soka safi na kushinda na ndicho kilichotokea leo, nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyofanya,” alisema Robertinho.

Kuhusu mashabiki kujitokeza kwa wingi, alisema wamekuwa wakiwapa sapoti na mara zote wanakuwa upande wao anawashukuru sana na kuendelea kuhakikisha anawapa furaha.

Alisema wanajiandaa kwa mechi yao ijayo dhidi ya Singida Fountain Gate FC kuhakikisha wanapata matokeo mazuri na kuendelea kusalia kuwepo kileleni.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WANIGERIA....MCHAMBUZI BONGO AWAKUMBUSHA YANGA SC MAMBO YA SIMBA..