Hassan Mwakinyo
Habari za michezo

PAMOJA NA KUFUNGIWA KUCHEZA NGUMI…MWAKINYO AIBUKA NA ‘KUSANUKA’ NA HILI JIPYA…

admin October 10, 2023 7:43 pm

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imemfungia Bondia Hassan Mwakinyo kujihusisha na mchezo wa ngumi nje na ndani ya Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja na faini ya Tsh milioni 1.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kugomea pambano lake lililokuwa lifanyike Septemba 29, 2023, Dar es Salaam dhidi ya mpinzani wake Julius Indongo kutoka nchini Namibia.

Siku moja kabla ya maamuzi hayo kutolewa, kupitia mitandao binafsi ya kijamii ya Hassan Mwakinyo aliandika maneno yafuatayo:

“Nilielewa mapema sana huu mchezo mchafu, nia ovu pamoja na dhamira zenu na hatma iliyotengenezwa kwa thamani ya pesa, nafikiri sasa bila kupepesa macho tunalazimika kuweka vitu wazi wazi hadharani kwenye hili.

“Ili inapotokea tena ishu kama hii kuwe na adabu ya maamuzi hususani kwenye mchezo wetu, ni kweli pesa inaweza nunua haki na utu wa mtu lakini hio ni kwa mtu ‘boya’ asiyejuwa thamani na haki zake za msingi… see you soon…”

YA COUTINHO NA LIVERPOOL YAKE YASIJE KUMKUTA LUIS MIQUISSONE….ISHU NZIMA IKO HIVI… ‘KAZI CHAFU’ ZA CHE MALONE NA KENNEDY JUMA ZAMFANYA MBRZAILI SIMBA KUFUNGUKA HILI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply