Habari za Simba SC
Habari za michezo

ROBERTINHO AONA ISIWE TABU AONGEZA BEKI MWINGINE

Staff Desk October 10, 2023 2:32 pm

Kocha mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema baada ya timu yake kuwa na uwezo wa kufunga kila mechi, bado kuna tatizo la mawasiliano katika safu ya ulinzi licha ya Che Malone Fondoh na Kennedy Juma kucheza vizuri.

Robertinho amesema; “Kwa muda mrefu tumekuwa tunamtumia Inonga (Henock), lakini sasa hayupo tunawatumia Che Malone na Kennedy, Wanafanya kazi kubwa, lakini tunatakiwa kuwaongezea kitu.

“Tunaweza kufunga mabao, lakini tunatakiwa kuongeza umakini na kuimarisha mawasiliano mazuri na mabeki wetu, ili wasiruhusu mabao katika mechi zijazo kwani zitakuwa ni mechi ngumu.

Robertinho ameongeza watatumia muda wa mapumziko wa kalenda ya kimataifa kuwaongezea ubora mabeki kabla ya kurudi kwenye mechi zijazo;

“Hizi siku nitakaa nao ili kuondoa makosa niliyoyaona katika michezo hii ya ligi kwani sikuweza kuwabadilisha kutokana na ratiba ngumu ya mfululizo wa mechi zilizokuwepo.

“Naamini bado tunaweza kufanya vizuri kabla ya mechi ya Super League dhidi ya Al Ahly na Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Robertinho.

AHMED ALLY ATAMBA KUHUSU UBINGWA, KUHUSU SOKA BIRIANI AWAPA NENO HILI MASHABIKI YANGA YAWEKA WAZI NGUZO TANO, NBCPL, CAFCL

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply