Habari za Simba
Habari za michezo

MBRAZILI SIMBA ATAMBA ‘KUZIFUMUA’ TIMU ZOTE LIGI YA MABINGWA AFRIKA…

admin October 13, 2023 11:21 am

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’, amefunguka kuwa, amefuatilia timu anazokutana nazo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kudai anaamini kikosi chake kitafanya vizuri kwa kuwafunga wote.

Katika michuano hiyo, Simba imepangwa Kundi B na timu za Wydad Casablanca ya Morocco, ASEC Mimosas (Ivory Coast) na Jwaneng Gallaxy (Botswana).

Mechi za hatua ya makundi zinatarajiwa kuanza kati ya Novemba 24 na 25, mwaka huu ambapo kila timu lazima zikutane mara mbili nyumbani na ugenini, kisha zile mbili za juu zitafuzu 16 bora pindi hatua ya makundi ikikamilika.

Robertinho amesema kuwa, Simba ni miongoni mwa timu kubwa Afrika, hivyo wana furaha kucheza mechi ngumu kama hizi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo alisisitiza kuwa, kwenye kikosi chake, kuna wachezaji wenye kiwango kizuri na anaendelea kuwasuka vijana wake kupata matokeo mazuri zaidi nyumbani na ugenini.

“Tuna mikakati mizuri kuelekea mechi hizo, katika histori Simba iliwahi kucheza na timu zote, ikiwemo Wydad Casablanca ambayo hapa tulipata matokeo mazuri nyumbani na kwenda kupoteza ugenini.

“Kazi kubwa kwa sasa ni kuandaa timu ambayo itapata matokeo mazuri nyumbani na ugenini ili kutafuta alama za kwenda hatua ya robo fainali ya Afrika,” alisema Robertinho.

RATIBA YA SIMBA CAF

NOVEMBA 24–25, 2023

Simba v ASEC Mimosas

DESEMBA 1–2, 2023

Jwaneng v Simba

DESEMBA 8–9, 2023

Wydad AC v Simba

DESEMBA 19, 2023

Simba v Wydad AC

FEBRUARI 23–24, 2024

ASEC v Simba

MACHI 1–2, 2024

Simba v Jwaneng Galaxy

HII HAPA BIASHARA YENYE FAIDA KULIKO….UTAPEWA MPAKA 10% YA DAU LAKO NDANI YA MERIDIANBET.. CAF WAPANGA ‘MAPROO’ BONGO KUKIPIGA DHIDI YA TAIFA STARS…MCHONGO MZIMA UKO HIVI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply