Habari za Michezo
Habari za michezo

WAKATI MBRAZILI SIMBA AKISUBIRI MUDA UFIKE…KOCHA AL AHLY AANZA KUWEWESEKA…

admin October 19, 2023 5:45 pm

Kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema maandalizi yamekamilika na sasa kikosi chake kinasubiri muda ufike wakatafute alama tatu dhidi ya Al Ahly kesho Oktoba 20 katika dimba la Mkapa saa 12:00 jioni.

Michuano ya African Football League (AFL) imelenga kukuza, kurithisha na kulipa thamani soka la Afrika ambapo katika msimu wake wa kwanza ambao unazinduliwa rasmi kesho itahusisha timu nane pekee, ambazo zimechaguliwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ubora na umaarufu wa klabu lakini kwa msimu utakaofuata timu zitaongezeka na kuwa 22.

“Ni mechi ngumu kwetu lakini tumejiandaa kushinda, ni wa kati wetu kuionyesha dunia ukubwa tulionao na naamini kesho, kila mtu ataiona Simba ikishinda,” alisema Robertinho ambaye wachezaji wake wote wapo kambini wakiingoja mechi hiyo.

Kwa upande wa kocha wa Ahly Marcel Koller alisema anajua ugumu wa Simba na anaamini anakuja kucheza na timu inayokamia.

“Simba inatimu nzuri, najua watacheza kwa kukamia lakini tumejiandaa kuwakabili,” alisema Koller

KUELEKEA MECHI YA KESHO….SIMBA WAMVIKA ‘MABOMU MAALUMU’ KIBU DENIS…UKWELI UKO HIVI… KUELEKEA MECHI YA KESHO….BOCCO APIGWA STOP…MBRAZILI SIMBA APEWA ‘KIMEMO’ ASIMPANGE KABISA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply