Habari za michezo
SIMBA HAKUNA KUPOA KUSEPA LEO JIONI KUWAFUATA AL AHLY
Staff Desk
October 21, 2023
4:50 pm
Kikosi cha Simba SC kinatarajia kuondoka nchini jioni hii ya leo Oktoba 21, 2023 kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kuvaana na Al Ahly.
Simba wanakwenda Misri kuvaana na Al Ahly baada ya kulazimishwa sare ya goli 2-2 kwenye mchezo wa robo fainali ya kwanza ya mashindano ya African Footbal League.
“Tunakwenda Misri sio kinyonge maana hakuna cha kututisha, tulicheza vizuri hapa nyumnani lakini matokeo yametusaliti lakini tunakwenda kule kumalizia kazi,” alisema Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.