Habari za Yanga SC
Habari za michezo

GAMONDI AWEKA WAZI SIRI YA YANGA KUPATA MATOKEO MAZURI MARA KWA MARA

Staff Desk October 25, 2023 12:08 pm

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi ameeleza kuwa timu yake inapata ushindi mkubwa na kwenye mechi ngumu kwa sababu wachezaji na timu yake wanacheza kibingwa.

Gamondi alisema, anafurahishwa na namna ambavyo wachezaji na timu yake inavyocheza, hiyo inamfanya aone kabisa kuwa wanakwenda kutimiza malengo yao msimu huu.

“Timu inacheza kibingwa sana, kuna wakati unakuwa hauna wasiwasi kama kocha, kwenye mechi ngumu ugeuka na kuwa mechi rahisi. Hiyo kwetu inatia faraja kama benchi la ufundi.

“Unaweza ukaona mechi yetu na Azam FC, tulijua kuwa itakuwa ngumu sana kwa kuwa wapinzani wetu nao ni bora, lakini mwisho wa mchezo tunashinda na kuifanya mechi ionekane kama rahisi. Nawapongeza sana wachezaji wangu,” alisema Gamondi

UKIACHANA NA JACKPOT YA MIL 200, KUNA MGAO WA MIL 2 KWA KILA MTU NDANI YA MERIDIANBET.. HIKI HAPA NDIO KILICHOMPONZA ROBERTINHO MBELE YA AL AHLY

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply