Taifa Stars
Habari za michezo

MAJANGA MKUDE AMFUNGULIA MASHTAKA MO DEWJI ADAI FIDIA KISA HIKI HAPA

Staff Desk October 26, 2023 3:16 pm

Mchezaji wa Klabu ya Yanga, Jonas Mkude amefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiidai Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) fidia ya Sh 1 bilioni kwa kutumia picha zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na Twitter bila idhini yake.

Mkude amefungua kesi ya madai 192 ya mwaka 2023 mbele ya Jaji Butamo Philip dhidi ya kampuni hiyo akiidai fidia hiyo Kwa kuvunja haki yake ya msingi.

Mkude amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Simba aliyotumikia kwa misimu 12.

Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL) yako chini ya Rais wa Heshima wa Simba Mohammed Dewji.

ALIYELETA JEZI FEKI SIMBA, YANGA KUANIKWA HADHARANI LEO KWA HAKIKA YA ASILIMIA 100 YA USHINDI IKO KWENYE SLOT HII NDANI YA MERIDIANBET…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply