Habari za michezo
DUKE ABUYA AIPIGA MKWARA YANGA
Staff Desk
October 27, 2023
8:28 am
Nyota wa Singida Big Stars, Duke Abuya amesema ni muda kwao wa kuonyesha ubora wao mbele ya Yanga kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
“Kila mchezo ni mgumu kama iliyopita na sisi wachezaji jukumu letu ni kuhakikisha tunapambana kwa ajili ya timu, hii ni nafasi nyingine ya kuonyesha ukubwa tuliokuwa nao kwa sababu uwezo na uzoefu tunao wa kukabiliana na yeyote,” alisema.
Duke aliyesajiliwa akitokea Police FC ya Kenya aliongeza ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo katika mchezo uliopita, umewaongezea morali kubwa huku akianisha licha tu ya kuiheshimu Yanga kutokana na ubora wao ila hawatoingia kinyonge.
“Tunaiheshimu Yanga ila hatotakuja kinyonge kwani tunahitaji kupata pointi tatu pia,” alisema. Singida tangu imepanda haijawahi kuifunga Yanga
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.