Home Habari za michezo HUU HAPA ‘UCHAWI’ WA AZIZI KI KUWA MOTO MSIMU HUU NDANI YA...

HUU HAPA ‘UCHAWI’ WA AZIZI KI KUWA MOTO MSIMU HUU NDANI YA YANGA….BALAA LAKE SIO POA..

Habari za Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI amesema anaiona timu hiyo ikifunga idadi kubwa ya mabao msimu huu tofauti na msimu uliopita kutokana na kutokumtegemea mchezaji mmoja.

Yanga hadi sasa ina mabao 20 kati ya hayo ni matatu tu yamefungwa na nafasi tofauti na kiungo ambayo ni bao la Dickson Job, Keneddy Musonda na Hafiz Konkoni mengine yote yamefungwa na viungo.

Aziz Ki amesema kocha Miguel Gamondi ametengeneza timu ya ushirikiano na kuhakikisha inatafuta pointi tatu muhimu bila kujali nani atafunga siku hiyo

“Yanga ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kuona goli hivyo kila anayepata nafasi ya kucheza anaingia uwanjani akiwa na akili ya kuipambania timu kupata matokeo mazuri apambane kufunga na kuzuia hili kwa asilimia kubwa limefanikiwa;

“Naweza nikakosa nafasi ya kufunga akafunga Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Clement Mzize, ukiangalia hadi mabeki wanafunga, hivyo kazi yao sio kulinda tu wanatakiwa kupanda kutengeneza mashambulizi pia wakipata nafasi wafunge kama ilivyo kwa Job,” amesema.

Aziz Ki amesema umoja walioutengeneza ndio siri kubwa ya kucheza kwa kujiamini na kutumia vizuri nafasi wanazozipata akikiri kuwa msimu uliopita haikuwa hivyo kwasababu walikuwa wanaamini katika kumtengenezea nafasi mshambuliaji tu.

Amesema Gamondi amewapa akili kubwa ambayo inawatesa wapinzani wao kila wanapokutana kwani wakimkaba yeye kwa kuamini kuwa ndiye atakayewaadhibu anafunga mchezaji mwingine ambaye hawajamtarajia.

“Hakuna raha ya kucheza mpira bila presha kutoka kwa wapinzani kama ilivyo Yanga ya sasa tunafanya kile ambacho tunaelekezwa na kocha na kimekuwa kikitulipa ubora wetu ni kutokana na kutokujipa umuhimu tunapokuwa uwanjani kila mmoja anachukuliwa kujua anachokifanya uwanjani.” amesema kiungo huyo kinara wa upachikaji mabao.

Aziz KI ambaye ametupia mabao sita hadi sasa kwenye mechi saba amesema malengo yao ni kutetea ubingwa na kufunga idadi kubwa ya mabao ili kujenga mwendelezo mzuri eneo hilo ambalo amekiri kuwa na mastaa wengi wenye uwezo.

Mabao 20 ya Yanga yamefungwa na Job, Hafiz, Yao, Musonda wote bao moja moja, Pacome (3), Aziz Ki (6), Mudathir (2), Maxi Zingeli (5).

Yanga itakutana na watani zao Simba, iikiwa imekusanya pointi 18 sawa na Simba ambayo ipo nyuma kwa mchezo mmoja.

SOMA NA HII  BENCHIKHA APIGA STOP USAJILI WA CHARAMBA SIMBA....ISHU NZIMA ILIANZIA HAPA...