Home Habari za michezo KISA YANGA KUCHEZA KWA MKAPA KESHO ….JEMEDARI SAID ATUPA DONGO HILI KWA...

KISA YANGA KUCHEZA KWA MKAPA KESHO ….JEMEDARI SAID ATUPA DONGO HILI KWA TFF…

Habari za Yanga

Wakati Yanga wakihamisha mchezo wao dhidi ya Azam FC kutoka katika Uwanja wa Chamzi kuja Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Oktoba 23.

Mchambuzi wa Michezo kutoka Efm, Jemedari Said anasema;

“Kama unataka kuhamisha mechi yako ya nyumbani baada ya kuthibitisha uwanja wa nyumbani wakati kabla ya Ligi kuanza unapaswa kuwa na sababu nzito na za msingi, utambulisho wa namna hii pia unafanywa wakati wa kuthibitisha kiwanja chako cha nyumbani na kushiriki Ligi au katika mazingira maalumu na unatoa taarifa kwa Bodi ya Ligi Kuu siku Saba (7) kabla ya tarehe ya mchezo husika.

Lakini zile mechi mbili ambazo klabu inaruhusiwa kucheza nje ya uwanja wake wa nyumbani, kanuni inasema hivyo viwanja kwanza visiwe vinatumika kwa Ligi Kuu, lakini pia unapaswa kuwasilisha uteuzi wako wa viwanja hivyo siku ishirini na moja (21) kabla ya tarehe ya michezo hiyo unayopanga kucheza katika viwanja husika.

Mabadiliko ya mchezo wa Yanga na Azam yamefanyika jana na kuthitibishwa na Bodi ya Ligi Kuu @ligikuu ambapo ni siku siku 4 tu kabla ya siku ya mchezo kinyume na kanuni ambapo inahitaji walau siku 7?

Bodi ya Ligi Kuu kwa makusudi IMESIGINA KANUNI yake na KUIPENDELEA YANGA kuhamisha mchezo wake dhidi ya Azam kinyume na kanuni. Bodi hii hii iliikatalia Simba kuhamisha mchezo wake dhidi ya Coastal Union siku chache kabla mchezo wa marejeo na Power Dynamos ya Zambia kwenye kufuzu CAFCL ikisimamia kanuni, leo kanuni imekiukwa hii ni hatari sana kwenye soka letu.

Bodi inapaswa kusimamia kanuni bila kuleta shaka shaka ya upendeleo kwakuwa ni chombo kinachosimamia timu zote na kuweka weledi mbele. Mpaka juzi Yanga walikuwa wanatangaza mechi yao itafanyika Chamazi siku ya Jumapili, jioni kukaja taarifa za mechi kuchezwa Jumatatu hukohuko Chamazi, jioni kama sio mchana jana kukawa na taarifa rasmi ya mechi kuchezwa Benjamin Mkapa kinyume cha Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2023.

Kuna wakati mnafanya mambo kienyeji mnatutafuta tu maneno muache kutusalimia, ila mnafanya mambo ya hovyo sana kiasi tunashindwa kuamini kama ni nyinyi tunaowafahamu tangu zamani, mnaojinasibu kufanya kwa weledi. Yanga watacheza mechi 2 kwenye uwanja wa Mkapa kabla mechi ya Derby, Simba wanacheza leo halafu wakirudi watacheza Uhuru kabla ya Derby pale kwa Mkapa, je mko sahihi?

SOMA NA HII  RAIS WA FIFA NA MASTAA WA SOKA KUTUA TANZANIA...KARIA AFUNGUKA 'SHOW' NZIMA ITAKAVYOKUWA...