Habari za Yanga SC
Habari za michezo

METACHA NDIO BASI TENA YANGA….GAMONDI ‘ASIMAMIA UKUCHA’ JAMBO LAKE…

admin November 2, 2023 12:42 pm

Imeelezwa kuwa mlinda lango Metacha Mnata bado hajarejea kikosini baada ya kocha Miguel Gamondi ‘kumuwekea ngumu’ kurejea kikosini hapo kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kurudi kutoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Nidhamu ya wachezaji ni kipaumbele cha kwanza cha Gamondi na amekuwa mkali kwa wachezaji ambao hawafuati taratibu zilizowekwa.

Metacha alichelewa kujiunga na kikosi cha Yanga baada ya majukumu ya timu ya Taifa na alitakiwa kutoa maelezo kwani hakutoa sababu mapema kwa nini amechelewa.

Kwa sasa bado hayuko sehemu ya kikosi akikosa mechi tatu zilizopita kwenye ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc, Geita Gold na Azam Fc.

Djigui Diarra na Aboutwalib Mshery ndio walinda lango wanaoonekana kwenye mazoezi ya Yanga.

SHAFFIH DAUDA:- MADHAIFU YA SIMBA YAPO KWA INONGA…CHE MALONE ANAZIBA MAKOSA YAKE… WATZ WASHINDA ZAIDI YA BILIONI 53 KWA SIKU 10 NDANI YA BETPAWA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply