Habari za Simba SC
Habari za michezo

KAMA HALI ITAENDELEA HIVI SIMBA HAINA NAMNA NI KIPIGO TU

Staff Desk November 10, 2023 11:36 am

Kikosi cha Simba SC kimeendelea kuharibu ubao wake baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo FC, mchezo uliopigwa jana katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Upepo wa kipigo cha bao 5-1 kutoka kwa Yanga weekend iliyopita kimechafua kabisa hali ya hewa ndani ya Kikosi cha Simba na kusababisha kumtimua kocha wao, Robertinho pamoja na kocha wa viungo, Hetegekimana Corneille.

Bodi ya Ligi imeusogeza mbele mchezo wa Simba dhidi ya Azam FC, vinginevyo aibu nyingine ingewakuta Simba kwa hali inavyoonekana sasa hivi.

Katika michezo 12 ambayo Simba imecheza msimu huu (Ligi pamoja na michuano ya kimataifa), ni michezo miwili tu ambayo hawajaruhusu bao, lakini michezo 10 yote wameruhusu nyavu zao kutikiswa.

Tatizo kubwa linaonekana kwenye safu ya ulinzi ya Simba ambayo inaruhusu mabao karibu kila mechi ambapo mpaka sasa kwenye michuano yote, Simba wamefunga mabao 24, na kuruhusu kufungwa mabao 17.

Matokeo ya Simba msimu huu;
◎ Simba SC 4 – 2 Mtibwa ›› (A)
◉ Simba SC 2 – 0 Dodoma Jiji (H)
◎ Simba SC 2 – 2 Dynamos ›› (A)
◉ Simba SC 3 – 0 Coastal Union (H)
◎ Simba SC 1 – 1 Dynamos (H)
◎ Simba SC 3 – 1 Prisons ›› (A)
◎ Simba SC 2 – 1 Singida FG ›› (A)
◎ Simba SC 2 – 2 Al-Ahly
◎ Simba SC 1 – 1 Al-Ahly ›› (A)
◎ Simba SC 2 – 1 Ihefu FC (H)
◎ Simba SC 1 – 5 Yanga SC (H)
◎ Simba SC 1 – 1 Namungo FC (H).

Unakionaje kiwango cha Simba watachukua ndoo ya Ligi Kuu?

ALIYECHUKUA MIKOBA YA ROBERTINHO AZUNGUMZIA SARE YA JANA HUU NDIO WAKATI WA MASHABIKI WA SIMBA KUFNYA MAMUZI MAGUMU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply