Habari za Simba leo
Habari za michezo

WAKATI MO DEWJI ‘AKIPUNGUZA JOTO’ MSIMBAZI….TRY AGAIN KAIBUKA NA HILI KUHUSU KOCHA MPYA…

admin November 15, 2023 5:46 pm

Rais wa Heshima wa Simba SC, Mohamed Dewji amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na minong’ono ya hapa na pale tangu kushuhudiwa #DerbyYaKariakoo Novemba 5, 2023.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Dewji ameandika

“Hakika pamoja na uzito, upo wepesi. WanaSimba: Naomba tutulie nakuwa-amini viongozi wetu”

Mbali na kuwaomba utulivu, pia Rais huyo wa Heshima amewaomba mashabiki kuendelea kufika uwanjani kuishabikia timu yao inapocheza.

Kwa upande Mwingine,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdalla ‘Try Again’ amesema ni kweli Simba inasaka kocha lakini watawatangazia mashabiki wao watakapompata kocha sahihi.

Akizungumzia suala la kocha wakati akihojiwa katika kituo cha Azam TV baada ya kutajiwa jina la Sven Vandenbroeck alisema ni kocha mzuri aliacha rekodi nzuri ndani ya Simba na amefanya mambo makubwa Morocco.

“Ni kocha mzuri lakini siwezi kusema ndiye anayeweza kuja kuinoa Simba ila mashabiki na wanasimba wanatakiwa kufahamu tutamleta kocha mzuri anayelifahamu soka la Afrika na Ligi ya Mabingwa;

“Lengo ni kuona anatuongoza kuanzia tulipo na kutufikisha sehemu kubwa ambayo tumekuwa tukiitamani muda mrefu hatua ya Nusu fainali Ligi ya Mabingwa na mchakato wake unaenda vizuri anaweza kuja kabla ya mchezo wetu wa hatua ya makundi nyumbani au baada,” alisema Try Again.

YANGA:- SIMBA WAKIENDA KUSHITAKI LOGO YAO KUTUMIKA, WASISAHAU NA ZILE GOLI 5 NI ZAO PIA… KIBOKO YENU ANAKUJA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply