Habari za Simba
Habari za michezo

KISA SAKHO SIMBA WAFUNGIWA KUSAJILI…… ISHU NZIMA IKO HIVI

Staff Desk November 23, 2023 4:00 pm

Klabu ya Simba SC, imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa madai ya klabu ya Teungueth ya Senegal kuhusu mcheza Pape Ousmane Sakho.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kutokana na mauzo ya Sakho. Kabla ya kujiunga na Simba, Sakho ambaye hivi sasa anachezea timu ya Quevilly Rouen Metrapole ya Ufaransa, alikuwa mchezaji wa Simba.

Klabu hiyo ilifungua kesi FIFA dhidi ya Simba ikidai sehemu ya malipo kutokana na mauzo ya Sakho. Simba ilitakiwa iwe imetekeleza uamuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa lakini haikufanya hivyo.

Wakati FIFA imeifungia klabu hiyo kufanya uhamishpo wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia Simba kufanya uhamisho wa ndani.

TFF inazikumbusha klabu kuheshimu sharia, kanuni na taratibu za mpira wa miguu ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili wachezaji.

TANZANIA INAPASWA KUAMINI VIJANA TIMU YA TAIFA… BASHIRI NA CHEZA KASINO USHINDE… YANGA WAANZA VISIGIZIO MAPEMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply