Habari za michezo

MASHABIKI WA SIMBA NA MSONGO WA KUKOSA MATOKEO MAZURI, WAISUSA SIMBA KWA MKAPA

Staff Desk November 26, 2023 9:34 am

Msongo wa kukosa matokeo mazuri bado inaonekana kuwakumba mashabiki wa Simba baada ya kuibuka kwa idadi ndogo kuipa nguvu timu yao.

Simba itashuka Uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa ikiwakaribisha ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikiwa limesalia saa moja kabla ya kuanza mchezo huo utakaoanza saa 10:00 jioni mashabiki wa Simba ndani ya uwanja sio wengi ambapo eneo kubwa la viti likiwa wazi.

Nje ya uwanja nako hakuna presha kubwa ya mashabiki kama ambavyo imezoeleka kwa Simba katika mechi za Kimataifa.

Simba haijapata matokeo mazuri kwenye mechi zake mbili zilizopita ambapo ilipoteza dhidi ya Yanga Novemba 5 kwa mabao 5-1 matokeo ambayo yaliwaumiza mashabiki wa timu hiyo kisha kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Namungo ya Lindi nyumbani.

Simba pia haijashinda mechi ya Kimataifa msimu huu ikikumbuka ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia katika mchezo ambao uliwavusha kuwapeleka hatua ya makundi kufuatia awali kupata sare ya mabao 2-2 na kufuzu kwa faida ya mabao ya ugenini.

UNAJUA SIMBA WALIMNASA VIPI BENCHIKHA….. MBINU ILITUMIKA HIVI JENGO LA YANGA LAPIGWA MNADA KISA HIKI HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply