Habari za michezo
DIARRA KAMA KAWA DHIDI YA AL AHLY
Staff Desk
November 28, 2023
10:59 am
Kipa wa Yanga SC, Djigui Diarra, anatarajia kuwepo katika mchezo ujao dhidi ya Al Ahly baada ya jana kukosekana tulipocheza dhidi ya CR Belouizdad.
Diarra aliukosa mchezo wa Ijumaa iliyopita kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya bega.
Kuelekea mchezo ujao dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Desemba 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Dokta Yusuf amesema kuna asilimia kubwa za Diarra kudaka.
“Tunafuatilia vyema maendeleo yake ya jeraha la bega na anaweza kuwa sehemu ya kikosi katika mchezo ujao,” alisema Dokta Yusuf.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.