Home Habari za michezo WACHEZAJI SIMBA WAKIRI KUVURUNDA….CHAMA APIGA MAGOTI KUOMBA MSAMAHA…

WACHEZAJI SIMBA WAKIRI KUVURUNDA….CHAMA APIGA MAGOTI KUOMBA MSAMAHA…

Habari za Simba

WACHEZAJI wa Simba wamekiri kukosea na kudai sasa wanafungua ukurasa mpya kwa kupambana na kupigania nembo ya klabu hiyo kuhakikisha wanafikia malengo yanayotarajiwa na Wanasimba.

Nyota hao akiongozwa na kiungo Clatous Chama aliwaomba msamaha mashabiki wa timu hiyo kwa matokeo ya mechi tatu zilizopita kwa kutocheza vizuri na hawakustahili kupata matokeo hayo.

Simba ilipoteza mechi dhidi ya Yanga bao 5-1, ikaja kupoteza alama mbili kwa sare ya 1-1 na Namungo FC katika Ligi Kuu Bara na sare ya matoko ya bao 1-1 katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, majuma yaliyopita uwanja wa Benjamin Mkapa Dar.

Chama alisema baada ya matokeo ya mechi yao na Asec Mimosas walikaa, wamejiuliza na kuona makosa yao na kuhakikusha haitajirudia kwa kuwaahidi mashabiki kufanya vizuri kwenye michezo iliyopo mbele yao.

“Hakuna ugomvi kati ya uongozi na wachezaji ni upepo mbayq umepita kwetu, tukumbuke msimu uliopita tulipoteza dhidi ya Horoya FC ugenini na Raja Casablanca hapa nyumbani lakini tulitulia na kufanya vizuri hadi kufika robo fainali ya ligi ya mabingwa,” alisema Chama na aliongeza kuwa :

“Simba timu kubwa na matarajio yake ni kufanya vizuri kila mashindano ili kufikia malengo, tumepitia katika kipindi kigimu, kama timi hatupaswi kuonyesha vidole badala yake tuwe pamoja na hatimaye tuvuke na kurejea katika kipindi cha furaha,” alisema kiungo huyo na kuwataka mashabiki kutokata tamaa na kuendelea kuwasapoti kuja uwanjani kwa wingi.

SOMA NA HII  SIMBA YAZIDI KUNOGA DILI JENGINE LA KIBABE LATIKI MCHEZAJI HUYU UHAKIKA KUKIPIGA SIMBA