Habari za Simba SC
Habari za michezo

WAKATI EDO KUMBWEMBE ‘AKIMPAKA’ BENCHIKHA….AHMED ALLY KAMJIBU HIVI….

admin December 5, 2023 1:55 pm

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mara baada ya Simba kuanza kufundishwa na kocha wao mpya Benchikha, mazoezi yake yanavutia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ahmed ameweka ujumbe huo akionesha ana hamu ya kwenda kuangalia mazoezi ya Benchikha.

“Muda ufike tuu tuende mazoezini siku hizi raha kweli kuona mazoezini yetu. Raha unayoipata kuiona Simba ya Benchikha ni kama kupokea mshahara au kuvunja kikoba.”

Aidha katika hatua nyingine,Mchambuzi wa soka nchini Edo Kumwembe amesema, tabia au hulka ya viongozi wa Simba na kocha wao mpya Benchikha zinafanana sio watu wa uvumilivu.

Amesema Benchikha akiona unamzingua hakawii kukuachia timu kama ilivyo kwa uongozi wa Simba, wanasifikika kwa kutimua walimu.

“Simba na Benchikha wana tabia sawa, ndio maana unaona Bechikha kashahama vilabu vingi, Raja kafundisha mara mbili sijui hivyo wana tabia sawa,” alisema Edo.

KWA NINI ZIMBWE Jr NI ‘MTI MKAVU’ SIMBA….UKWELI WA MAMBO UKO HIVI…JAMAA HALI KUKU KABISA… BAADA YA KUCHAGULIWA KUWA BOSI WA VILABU AFRIKA…MAJUKUMU YA HERSI HAYA HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply