Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

OYAA EEE MSIMCHUKULIE POA LAKRED ….. UONGOZI SIMBA NAO WATIA NENO

Staff Desk December 11, 2023 4:33 pm

Meneja wa idara ya habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally, ametoa taahadhari kwa mashabiki wanaobeza uwezo wa mlinda lango wao raia wa Morocco Ayoub Larkred na kusema ni nyanda mkubwa.

“Ayoub ni kipa mkubwa msimchukulie poa, ni kipa mkubwa mno, anaheshimika Morocco, ni mmoja wa makipa mwenye wasifu mkubwa nchini humo, muda unavyozidi kwenda uwezo wake wa kujiamini unazidi kupanda, muda si mrefu wana Simba watafaidi matunda yake” alisema Ahmed kwa kutamba kwenye video aliyochapisha kwenye mtandao wake wa kijamii.

Kwenye mchezo dhidi ya Wydad AC, licha ya Simba kupoteza 1-0, nyanda huyo alikuwa kwenye kiwango bora sana akiokoa michomo 5 kati ya mashuti 6 ya Wydad yaliyolenga lango huku mmoja ukiwa mkwaju wa penalti.

HAWA AZAM FC TUTAJUANA HUKO HUKO MBELE YA SAFARI SAKATA LA YANGA KUNG’OA VITI JAMBO LINAMALIZWA HIVI WIZARA YATOA TAMKO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply