Habari za Simba
Habari za michezo

ALICHOSEMA BENCHIKHA BAADA YA KUWABUTUA KAGERA 3-0…ALIA NA UWANJA…

admin December 15, 2023 10:14 pm

Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amewasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Benchikha amesema uwanja haukuwa rafiki kiasi cha kuwanyima kucheza soka safi lakini hata hivyo amefurahi kwa ushindi huo mnono.

Aidha Benchikha amesema Kagera ni timu nzuri na waliwapa ushindani mkubwa pamoja na kuwa walikuwa bora na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo.

“Tumecheza vizuri, nawapongeza wachezaji wangu. Tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini uwanja haukuwa rafiki na kutunyima kucheza soka safi

“Kagera ni timu nzuri wanacheza soka safi na walitupa ushindani mkubwa ingawa sisi tulikuwa bora ndio maana tumepata ushindi,” amesema Benchikha.

KUHUSU USHINDI WA SIMBA LEO DHIDI YA KAGERA….HAYA HAPA YA NYUMA YA PAZIA YAKUYAJUA… UNAHANGAIKA KUPATA USHINDI KUPITIA CASINO….SLOT HII NI MKOMBOZI WA KWELI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply