Tetesi za Usajili Bongo
Habari za michezo

FARID MUSSA ‘ASUKUMIWA’ SIMBA….MABOSI YANGA WAMPA UKWELI KUWA HATAKIWI….

admin December 18, 2023 12:48 pm

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Farid Mussa yupo huru kusajiliwa na timu yoyote itakayohitaji saini yake ikiwemo Simba ambayo imepanga kukifanyia maboresho kikosi chake.

Hiyo ni kutokana na mkataba wake kufikia mwisho mwishoni mwa msimu huu akiwemo Chrispin Ngushi, Denis Nkane ambao hivi sasa wamepoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Kwa mujibu kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), mchezaji anaruhusiwa kufanya mazungumzo klabu nyingine mkataba wake ukiwabakiwa na miezi kabla ya kumalizika. Hivyo Farid yupo huru kwa sasa.

Kwa mujibu wa taarifa , kiungo huyo anatajwa kuwindwa na baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara, ikiwemo Singida Fountain Gate.

Mmoja wa Mabosi wa Yanga, amesema kuwa hadi hivi sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanywa kati ya kiungo na uongozi wa timu hiyo kuhusu kuongeza mkataba mpya.

Aliongeza kuwa uongozi unafanya mazungumzo na wachezaji ambao wapo katika mipango ya kocha pekee, waliojihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi cha timu hiyo.

“Singida Fountain Gates ndiyo timu ya kwanza inayotajwa kuwania saini ya Farid, ni katika kukiimarisha kikosi chake, hivyo mazungumzo ya siri yanayoendelea kati ya mchezaji na timu hiyo.

“Kama mazungumzo yakihenda vizuri, basi huenda akajiunga na timu hiyo, Farid amekosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza, hivyo ni bora akaondoka hapo kwenda kutafuta changaamoto nyingine,” alisema mtoa taarifa huyo.

Rais wa Yanga, Injia Hersi Said allizungumzia hilo hilo la usajili kwa kusema: “Hatutakubali kumuachia mchezaji ambaye yupo katika mipango ya timu, kwani hivi sasa tunatengeneza timu itakayoleta ushindani katika michuano ya kimataifa, lakini tutamuachia mchezaji ambaye hayupo katika mipango ya kocha.”

BAADA YA SIMBA KUANZA KUPATA USHINDI….MANGUNGU KAIBUKA NA HILI JIPYA… HUU HAPA USAJILI WA KWANZA WA BENCHIKHA SIMBA….NI VIFAA 4 VYA KAZI NA UBINGWA…..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply