Klabu ya Simba chini ya kocha Abdelhak Benchikha inaonekana kuanza kurejea kwenye ubora ambao umezoeleka ndani ya timu hiyo kwa misimu kadhaa nyuma ambapo siku za karibuni ubora wa timu hiyo ulionekana kupoteza.
Simba walifanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad Casablanca wa mabao mawili kwa bila na kuweza kufufua matumaini ya kufanya vizuri katika ligi ya mabingwa Afrika.
Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako.
Wekundu wa Msimbazi walionekana walianza kwa kuchechemea katika ligi ya mabingwa kwani hawakua wamepata matokeo ya ushindi katika michezo yao mitatu ya awali kabla ya kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Wydad Casablanca.
Klabu ya Simba mara kadhaa sasa imekua ikitinga hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika, Jambo la kushtua ulikua ni mwenendo wa klabu hiyo waliouanza nao msimu huu kwenye michuano hiyo maana ulikua unatoa taswira ambayo sio nzuri.
Baada ya Wydad Casablanca kufungwa na Simba katika dmba la Benjamin Mkapa na Simba sasa klabu hiyo imebakiza michezo miwili ili kujihakikishia kufuzu katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika, Ambapo michezo hio itakua baina ya Asec Mimosas ugenini na mchezo wa mwisho nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy.
Klabu ya Simba imejiwekea malengo ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika jambo ambalo wamekua wakilipigania kwa misimu takribani mitatu sasa, Japo msimu huu ilionekana kama wasingeweza kufuzu hata hatua ya robo fainali lakini ujio wa kocha Benchikha umeibua matumaini upya.
Pia kumbuka kuna kucheza JACKPOT ya Meridianbet ambayo inakufanya ushinde shilingi Milioni Mia Mbili, 200,000,000 kwa dau lako la shilingi 1000 pekee
ukibashiri kwa usahihi mechi zako 13. Nafasi ni yako ingia www.meridianbet.co.tz na uweke mkeka wako.
SOMA NA HII BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA JANA....MABOSI SIMBA WABISHA HODI KWA MAMELOD NA AL AHLY...