Habari za michezo

LIGI KUU SIO KITOTO TENA SIMBA,YANGA JUMAMOSI HII

Staff Desk December 21, 2023 2:56 pm

Baada ya kukamilisha majukumu yao ya Kimataifa kwa ushindi mnono, wawakilishi wa nchi katika mashindano ya Klabu Bingwa, Simba SC na Yanga SC, wanarejea kwenye Ligi Kuu ya NBC Jumamosi, Desemba 23, 2023.

Simba ambao walitoka kuwanyoa Wydad Casablanca, wao watakuwa wageni kwa KMC majira ya saa 10:00 jioni huku Yanga waliotoka kuwakaza Medeama watakuwa wageni kwa Tabora United saa 1:00 usiku.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Simba wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 22, Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 25.

Ikumbukwe, Yanga amecheza michezo 10, Simba amecheza tisa.

BENCHIKHA AWATULIZA WANASIMBA LICHA YA USHINDI AJA NA KAULI HII BENCHIKHA AWATULIZA WANASIMBA AFUNGUKA HAYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply