UONGOZI wa Simba umepokea mapendekezo ya kutakiwa kufanya usajili wa wachezaji watano hadi sita kipindi cha dirisha dogo ili kuimarisha kikosi chao.
Baada ya kupokea mapendekezo hayo katika nafasi hiyo akiwemo kiungo mkabaji, beki wa kati na mshambuliaji ambapo tayari mchakato unaendelea baada ya kufanikiwa kunasa saini ya Ladack Chasambi kutoka mtibwa kwa mkataba wa miaka mitatu.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema tayari Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amekutana na uongozi kukabidhi ripoti yake ambayo imeainisha mapendekezo katika maeneo ya usajili kuboresha kikosi.
Alisema watafanya usajili ya wachezaji kadhaa wasiopungua watano kuimarisha kikosi cha timu hiyo kwa kuongeza watu kwenye mapungufu ambayo Benchikha ameyaona.
“Viongozi wamepokea mapendekezo hayo na kufanyia kazi, ni kweli tunahitaji wachezaji kuimarisha kikosi chetu, tuliokuwa nao sio wabaya bali wanahitaji kujituma na kujitoa kiti ambacho tunakikosa katika timu yetu.
Tunatarajia kuongeza mashine ambazo zitaluja kusaidiana na hawao walikuwepo hapa, kama tutafanikiwa kukamilisha usajili wa nyota wapya mapema wataungana na timu visiwania Zanzibar katika kombe la Mapinduzi,” alisema.
Ahmed alisema kikosi cha timu hiyo inaingia kambini leo na kuendelea na mazoezi katika uwanja wao wa Mo Simba Arena kwa ajili ya mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka.
“Kikosi kinatarajia kuondoka Desemba 30 au 31 mwaka huu kuelekea visiwani humo na tayari kwa mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Jamhuri utakaochezwa, Januari Mosi, 2034.
Tunatarajia mashindano hayo kujiweka imara na kocha Benchikha kupata muda mzuri wa kufanya mazoezi na muda wa kukaa na wachezaji wake kwa kuona uwezo wa mmoja mmoja mbali na wale waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa,” alisema Meneja huyo.
Alieleza hakuna mchezaji Majeruhi zaidi ya Aubin Kramo ambaye yuko kwenye hatua ya mwisho ya matibabu yake baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.
“Wachezaji wote wako fiti , Kramo yupo kwenye hatua za mwisho za matiabu yake na tunatarajia mapema mwakani ataanza mazoezi ya nguvu na uwanjani,” alisema Ahmed Ally akiweka wazi juu ya Sakata la Mosses Phiri
Alisema hawajapokea barua au ujumbe wowote kuhusu mshambuliaji wake huyo ambaye anadaiwa kutaka kuondoka na kuhusishwa na timu mbalimbali kuhitaji huduma yake.
“Phiri ameingia katika siasa ambazo kiungo wetu Clatous Chama aliwahi kuingia miaka ya hivi karibuni kuhusishwa kutakiwa na klabu hapa nchini lakini kwa miaka yote anaitumikia Simba.
Phiri bado ana mkataba na Simba, hatujapokea barua yoyote kutoka kwa nyota huyo, kama anahitaji kuondoka atalazimika kurudi kwenye mkataba wake na kuangalia vipengele hata Simba ikitakiwa kumuacha anatakiwa kuangalia mkataba. Kiufupi Phiri yupo sana,” alisema Ahmed.
Alisisitiza kuwa mbali na kupewa adhabu ya kusimamishwa na kupelekea kwenye kamati ya nidhamu lakini kiungo huyo anaendelea na programu za mazoezi aliyopewa na benchi la ufundi pamoja na kulipwa stahiki zake ikiwemo mshahara wake.
“Chama amepata tuhuma za utovu wa nidhamu na amepelekwa katika kamati ya nidhamu, hatuna nia ya kuachana naye, hatuwezi kuachana na mchezaji ambaye bado ana mkataba na hatujapata hitimisho la adhabu yake ya utovu wa nidhamu.
Kwetu ni mchezaji muhimu kama ilivyo kwa wachezaji wengine na hata iyafika hatua ya kuamua kuachana naye basi ataondoka Simba kwa heshima zote,” alisema Ahmed.
Comment: muache kucha afanye yake tunamuamini sana kocha wa matawi Benchika