Habari za Simba
Habari za michezo

MWAMBA KAGOMA KUSEPA NANI ATOKE SIMBA !?

Staff Desk December 30, 2023 2:17 pm

Klabu ya Simba kwenye dirisha hili la usajili inahitaji kufanya maboresho kwa kufanya maingizo ya nyota wapya wa kigeni watakaokuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chao.

Ili maingizo hayo yafanyike ni lazima waachane na baadhi ya nyota wa kigeni kwani kikanuni tayari wametosha.Sheria za Ligi kuu zinaitaka klabu moja kuwa na wachezaji [12] pekee wa kigeni.

Nyota ambao walitakiwa kupunguzwa ni pamoja na Luis Miqquisone ambaye hajawa na makali tangu alipojiunga na kikosi hicho.Simba ilipanga kumtoa kwa mkopo ili akaimarishe kiwango chake lakini nyota huyo amegoma.

Luis amewaambia wadosi kuwa anataka kuendelea kusalia kikosini hapo na huenda akarejesha kiwango chake kama awali.

Kama mwamba kagoma nani atoke?

KISA MKATABA SAIDO AWAGOMEA VIGOGO SIMBA SINGIDA FG WAMUANDHIBU FEI TOTO…. SIO POA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply