Habari za Simba SC leo
Habari za michezo

MWENDA:- “NILIKUWA NAJIONA KAMA MTUMISHI HEWA SIMBA”….AMTAJA KAPOMBE TENA..

admin December 31, 2023 7:40 am

Beki wa Simba SC, Israel Mwenda amesema ujo wa Kocha mpya kutoka nchini Morocco Abdelhak Benchikha umemfanya ajihisi amezaliwa upya kutokana na kupewa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Kabla ya Benchikha, makocha waliopita Simba SC miaka ya karibuni ni Pablo Franco, Zoran Maki, Juma Mgunda na Roberto Oliveira Robertinho’ wote hawakumpa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Akizungumza kisiwani Unguja-Zanzibar, amesema kwa muda mfupi ambao timu imekuwa chini ya Benchikha amecheza zaidi ya mechi nne na kutoa mchango mkubwa kwa timu yake hadi kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa.

“Nilikuwa najiona kama mtumishi hewa nalipwa mshahara bila kufanya kazi lakini kwa sasa nafurahi kuwapo hapa na ni miongoni mwa wachezaji ambao wanaipigania Simba SC kufikia malengo yake msimu huu,” amesema Mwenda.

Beki huyo amesema hana shida na uwezo wa Shomari Kapombe lakini makocha waliopita hawakuwa na utaratibu mzuri wa kuwapa nafasi wachezaji wengine kutoa mchango wao kwa timu zaidi ya kutumia baadhi ya wachezaji ambao anaamini ni msaada kwake.

KWA NINI UNUNUE Infinix HOT 40 Pro DHIDI YA SAMSUNG GALAXY A14…JIBU LA KIUFUNDI HILI HAPA.. HIKI HAPA WALICHOPANGA KUKIFANYA SIMBA KWENYE UWANJA MPYA WA AMANI ZNZ….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply