Home Habari za michezo KISA CHAMA NA PHIRI WABAKI AU WASEPE…..NYUMA YA PAZIA KWA MABOSI WA...

KISA CHAMA NA PHIRI WABAKI AU WASEPE…..NYUMA YA PAZIA KWA MABOSI WA SIMBA HALI IKO HIVI…

Habari za Simba

Wachezaji kutoka Zambia Clatous Chama na Mose Phiri wameonekana kuipasua Simba SC, kwa baadhi viongozi kutaka waendelee kuwapo klabuni huku wengine wakisema waondoke zao.

Awali, ilielezwa kuwa baadhi ya wadau wa klabu hiyo wakiwamo baadhi ya viongozi na benchi la ufundi, walitaka ishu za wachezaji hao zimalizike haraka kwa kuwaacha waende zao, lakini imeonekana kizuizi ni mikataba yao.

Hivi karibuni ilitolewa taarifa ya kusimamishwa kwa Chama, huku Phiri ikielezwa ameandika barua ya kuomba kuondoka kwenye timu hiyo kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Hata hivyo, chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba SC kinasema kila kikao kinachohusu ishu hiyo, kimekuwa kikiwagawa wajumbe baadhi wakitaka wachezaji hao wabaki na wengine wakitaka waondoke.

Taarifa zinasema, Phiri bado yupo kwenye kikosi akiendelea na ishu zake kama kawaida, huku suala la Chama likiwa linasubiri Kamati ya Nidhamu na Maadili kulimaliza, huku chanzo kikisema barua bado haijafikia kamati hiyo inayoongozwa na Kamanda Mstaafu wa Jeshi la Polisi Seleman Kova.

“Kwa Phiri hakuna ishu, kwa kuwa hata klabu haijawahi kuzungumza jambo lolote kuhusu suala lake, na hata sisi hatujawahi kuona hiyo barua, labda kama watu waliamua tu kuzusha ndiyo maana hata mchezo wa mwisho alikaa kwenye benchi na mazoezini hajawahi kukosa.

“Ishu ya kukosa nafasi, ni ya mchezaji mwenyewe, anatakiwa kupambana, sasa kama utaona mchezaji anakosa nafasi anaomba kuondoka huyo siyo mpambanaji, inachotakiwa ni yeye kuonyesha juhudi na kila mmoja anamuamini Phiri kuwa ni mchezaji mzuri, nafikiri hata kwenye Kombe la Mapinduzi ataonekana, ingawa kwa hali ya kawaida anaonekana hana furaha, na amekuwa akiwatumia watu kutaka kuondoka.

“Chama kwenye Kombe la Mapinduzi ana asilimia ndogo sana, kwanza haendi mazoezini na anaonekana anawaza maisha nje ya Simba SC, lakini shida ni kwa kuwa ana mkataba hadi mwisho wa msimu, Simba SC hawawezi kumuacha kwa kuwa atalipwa fedha nyingi, lakini ofa ikitoka nje hata sasa naona atauzwa tu,” kimesema chanzo cha habari hii.

SOMA NA HII  CAF WARUDI TENA NA TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRIKA...SAFARI HII MAMBO YATAKWENDA NAMNA KIULAYA ULAYA ZAIDI...