Home Habari za michezo WAKATI WAKIWAFIKIRIA WAGANA…MAXI NZENGELI AIBUA JAMBO YANGA…AL AHLY WATIA NENO…

WAKATI WAKIWAFIKIRIA WAGANA…MAXI NZENGELI AIBUA JAMBO YANGA…AL AHLY WATIA NENO…

Habari za Yanga

Yanga inajiandaa kupaa zake kwenda Ghana kuwahi pambano la tatu la Kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama, huku nyota mahiri wa timu hiyo, Maxi Nzengeli akiwatuliza mashabiki wa klabu hiyo baada ya timu kuambulia pointi moja tu kwenye mechi za michuano ya CAF hadi sasa.

Yanga juzi usiku ililazimishwa sare ya 1-1 na Al Ahly ya Misri kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki moja tu tangu ipasuke 3-0 ugenini mbele ya CR Belouizdad ya Algeria na kuifanya timu hiyo iburuze mkia wa kundi hilo linaloongozwa na Al Ahly yenye pointi nne.

Hata hivyo, kwa kujua mashabiki wa Yanga ni kama wamekatwa stimu kwa kuona timu yao ikiwa inaupiga mwingi uwanjani mbele ya wapinzani na kushindwa kuibuka na ushindi, kiungo mshambuliaji, Maxi Nzengeli amewatuliza kwa kuwaambia wameshajua walipokosea na wanajipanga upya kuwapa raha.

Maxi ameonyesha kujutia kukosa kiwango kizuri kwenye mchezo huo wa juzi, akisema bado hawajakata tamaa, lakini akasema anaamini timu hiyo ina nafasi ya kusahihisha makosa kwenye mechi mbili zijazo dhidi ya Medeama ya Ghana kabla ya kusubiri kufunga hesabu mwakani ili kujua hatma ya kutinga robo fainali.

Maxi alisema Yanga bado ina nafasi ya kufanya vizuri ikiwemo hata kufuzu robo fainali na kwamba wanaenda Ghana wakiwa na akili moja tu ya kuibuka na ushindi mbele ya wenyeji wao, walioipasua CR Belouizdad kwenye mechi iliyopita ikiwa nchini humo, baada ya awali kulala 3-0 kwa Al Ahly, jijini Cairo.

“Nimeumia kutokana na kushindwa kucheza vizuri kama ambavyo nilitaka nicheze hii mechi (dhidi ya Al Ahly) lakini inatokea kwenye soka hatujakata tamaa bado akili yetu ipo kamili,” alisema Maxi na kuongeza;

“Tunarudi kwa nguvu mechi ijayo, haitajalisha tupo ugenini tutaenda kutafuta ushindi ili kurudi kwenye malengo. Kila mchezaji anataka kuona Yanga ikivuka kwenda robo na hii haiwezekani kama hatutapambana. Tupo tayari kwa vile mashabiki waendelee kutuunga mkono.”

KIUNGO AL AHLY

Wakati huo huo kiungo wa Al Ahly Allou Dieng ameshindwa kujizuia kwa kusema mbali na ishu ya hali ya hewa ya joto waliyokumbana nayo uwanjani wakati wakiumana na Yanga juzi, lakini ukuta wa wababe hao wa Tanzania uliwapa kazi, licha ya kuvuna alama moja ugenini.

Dieng alisema ukuta wa Yanga ndio eneo lililofanya kazi kubwa kuwazuia wasishinde.

Dieng alisema mabeki wa Yanga licha ya kosa moja walilofanya la kuwapa bao, lililofungwa na Percy Tau, lakini kiujumla mabeki walicheza kwa utulivu mkubwa na kuwapa wakati mgumu kupenya.

Kocha Miguel Gamondi juzi aliwatumia Yao Kouassi, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Ibrahim Bacca na Bakari Mwamnyeto eneo la ulinzi.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO TZ ILIVYOPELEKEA RONALDO NA MESSI KUKOSA TUZO ZA FIFA...SAMATTA AFANYA MAAMUZI MAGUMU....