Tetesi za Usajili Bongo
Habari za michezo

FISTON WA YANGA ANUKIA COSTAL UNION…DILI LAKE LIKO HIVI…

admin January 1, 2024 4:45 am

WAKATI Coastal Union ikiwa na mpango wa kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji katika dirisha hili la usajili, nyota wa zamani wa Yanga, Fiston Abdulrazak ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye orodha ya wagosi hao wa Kaya.

Tayari Coastal Union imeachana na wachezaji sita katika kipindi hiki baada ya mikataba yao kumaliza ambao na Daud Mbweni, Yakubu Abdullah, Fran Golubic, Juma Mahadhi, Balama Mapinduzi na Abdulswamad Kasimu.

Fiston ambaye ni mshambuliaji wa kati wa Kirundi anayecheza soka la kulipwa Kenya ametajwa kuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa timu hiyo ambao wanafanyia kazi mapendekezo ya benchi lao la ufundi linaloongozwa na Mkenya, David Ouma akishirikiana na Fikiri Elias.

Ouma anatajwa kufanya mazungumzo ya siri na mshambuliaji huyo jambo ambalo linaweza kurahisha kutua kwake Coastal Union.

Ikumbukwe ya kuwa kocha huyo alikuwa Mkurugenzi wa michezo wa Sofapaka kabla ya kufanya maamuzi ya kujiunga na Coastal, klabu hiyo ndiyo anayoichezea Fiston ambaye kwa mara ya kwanza kucheza Ligi Kuu Bara alikuwa na Yanga lakini hata hivyo alishindwa kuwika.

STRAIKA MPYA AZAM AWAZIDI MASTAA WOTE WA SIMBA NA YANGA KWA MSHAHARA… BAADA YA KUMSHUSHA STRAIKA MCOLOMBIA….AZAM FC ‘WALETA BALAA’ LINGINE BONGO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply