Habari za Yanga LEO
Habari za michezo

UTAMBULISHO WA OKRAH ULIVYOKUJA NA ‘MAZINGAOMBWE’ YA GOLI 5 KAMA ZA SIMBA JANA…

admin January 1, 2024 12:31 pm

MGENI mwenyeji, Okra Magic ni mali ya Yanga yeye ni winga raia wa Ghana ambapo anajiunga na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamond kwenye dirisha dogo.

Desemba 31 2023 Okrah alitambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar.

Katika mchezo wa funga 2023 ubao baada ya dakika 90 ulisoma Jamhuri 0-5 Yanga ambapo Crispn Ngushi alitupia mabao mawili, Kibwana Shomari bao moja, Clement Mzize bao moja na kamba ya tano ilifungwa na Skudu Makudubela.

Okra aliwahi kucheza kwa watani wa jadi wa Yanga, Simba jambo ambalo limefanya Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe kusema kuwa ni mgeni mwenyeji ndani ya Bongo.

“Ni mchezaji mzuri anatambua namna kazi inavyofanyika hivyo kikubwa ni kuona kwamba anaendelea kutoa burudani kwa Wananchi hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

UKWELI MCHUNGU…..TAIFA HALINA MBADALA SAHIHI WA SAMATTA NA MSUVA…KELVIN JOHN MHHH… KOCHA TAIFA STARS ALIVYOBADILI UPEPO WA MASHABIKI WA BONGO KUHUSU TIMU YA TAIFA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply