Habari za Michezo
Habari za michezo

WAKATI VYUMA VYA MAANA VIKIZIZI KUSHUKA TZ…CHAMA , FEI TOTO WATAJWA HUKO…

admin January 7, 2024 8:13 am

NI nadra kwa wachezaji kuwasifia mastaa wenzao wanaocheza katika ligi moja, lakini kwa Kenny Mwambungu wa KMC kwake sio ishu sana, baada ya kuwataja Feisal Salum wa Azam na Clatous Chama wa Simba kuwa ni wachezaji anaowakubali kwa ubora wa viwango vyao.

Kenny alisema kuwa, Chama na Fei Toto ni wachezaji wa kuigwa kwa aina ya uchezaji wao na jinsi wanavyojitoa kwa timu wanazozichezea.

Akianza kwa Chama alisema jamaa ana uwezo wa kufanya timu icheze kwa utulivu, kwani huwa hana presha uwanjani, akihusika pia kuisaidia timu kupata ushindi na kubwa zaidi ni matumizi ya akili kuliko nguvu ndiyo yanambeba na kumfanya amwelewe sana.

“Kwa mtazamo wangu, Chama kwa muda aliokaa na kucheza Ligi Kuu, ameonyesha kitu cha tofauti, anacheza kisasa zaidi, kuna muda ukimtazama akicheza unakuwa unajisikia burudani, analifanya soka lionekane kama ni kazi rahisi kwa kipaji alichonacho,” alisema na kuongeza;

“Licha ya ushindani wa kila timu kutaka kupata pointi, wakati mwingine soka ni burudani.”

Kenny aliyewahi kutamba na Mbeya City, alisema staa mwingine anayemkubali ni Fei Toto.

“Ni kweli kuna muda alikaa nje kipindi akapitia changamoto na timu yake ya zamani Yanga, kajitafuta kajipata anaendelea kufanya vizuri, kipaji hakijifichi.”

GAMONDI AISHTUKIA SIMBA MAPINDUZI CUP ….AWAITA MASTAA WOTE ALIOWATOSA DAR… BENCHIKHA AINGILIA KATI ISHU YA MIQUISSONE KUBAKI AU KUSEPESHWA SIMBA…MSIMAMO WAKE HUU HAPA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply