Habari za Simba leo
Habari za michezo

AHMED ALLY:- SIMBA ILIKUWA HAINA NAMBA 6 ASILI….

admin January 7, 2024 8:30 am

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema usajili wa kiungo mkabaji, Babacar Sarr utaenda kutibu matatizo yote ya kiulinzi ya timu .

Ahmed amesema katika miaka ya karibuni Simba wamekuwa wakikosa namba sita asilia lakini baada ya Sarr kutua tatizo limetatuliwa.

Ahmed ameongeza kuwa tangu alivyoondika James Kotei, Gerson Fraga na Taddeo Lwanga Simba haijawahi kupata kiungo halisi wa ukabaji ndio maana wamepambana kupata saini ya Sarr.

“Sarr ni mchezaji ambaye tulikuwa tunamkosa katika timu yetu kwa muda mrefu. Tumekuwa na wachezaji wengi bora lakini hakutuwa na namba sita halisi.”

“Sasa pale kati patakuwa na Sarr, Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis, imani yetu ni kwamba tutakuwa na safu bora sana ya kiungo,” amesema Ahmed.

BENCHIKHA AINGILIA KATI ISHU YA MIQUISSONE KUBAKI AU KUSEPESHWA SIMBA…MSIMAMO WAKE HUU HAPA.. KUELEKEA MECHI NA APR LEO…..MASTAA YANGA WAJIFUNGA ‘MSHIPI’ MAPEMAA…..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply