Taifa Stars leo
Habari za michezo

HAWA HAPA MASTAA WANNE WALIOTEMWA TAIFA STARS KIKOSI CHA MWISHO AFCON 2023…

admin January 7, 2024 8:59 pm

Kipa Metacha Mnata na mshambuliaji Abdul Selemani ‘Sopu’ ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Taifa Stars ambao hawajajumuishwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka huu huko Ivory Coast.

Kwa mujibu wa orodha ya vikosi vya timu zote 24 zitakazoshiriki fainali hizo iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Sopu anayechezea Azam na Metacha wa Yanga, hawamo katika majina ya wachezaji 27 walioorodheshwa katika kikosi cha mwisho cha Taifa Stars.

Mbali na Sopu na Metacha, wengine wawili ni Khleffin Hamdoun na Twariq Yusuf.

Wanne hao walikuwa miongoni mwa wachezaji 31 wa Taifa Stars ambao wapo kambini kujiandaa na fainali hizo lakini kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya Afcon, idadi ya wachezaji wanaohitajika kikosini ni 27.

MZIKI WA AZAM FC WAMTISHA MSAUZI WA SINGIDA FG…KESHO UBISHI WOTE KWISHA… BENCHIKHA APIGA STOP USAJILI WA CHARAMBA SIMBA….ISHU NZIMA ILIANZIA HAPA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply