Habari za Michezo leo
Azam FC

MZIKI WA AZAM FC WAMTISHA MSAUZI WA SINGIDA FG…KESHO UBISHI WOTE KWISHA…

admin January 7, 2024 8:52 pm

KOCHA Mkuu wa Singida Fountain Gate, Msauzi Thabo Senong amewataka wachezaji wa timu hiyo kuongeza umakini na kuepuka makosa yanayoweza kuwagharimu wakati kikosi hicho kitakapopambana na Azam FC kesho katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 10:15 jioni unatazamiwa kuleta ushindani mkubwa na wa aina yake kutokana na ubora wa wachezaji wa timu zote mbili.

“Tumekuwa na siku chache za kurekebisha kasoro ndogondogo zilizojitokeza katika mchezo wetu wa mwisho na nawashukuru wachezaji wameonyesha kuguswa, hivyo kuniahidi kupambana zaidi kadri ya uwezo wao ili tupate matokeo mazuri,” alisema.

Senong alisema kitendo cha kupoteza mchezo wa mwisho dhidi ya Simba kwa kufungwa mabao 2-0, ilikuwa ishara tosha kuonyesha bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kutwaa taji hilo hasa wanapocheza na timu kubwa zenye wachezaji wazuri.

“Kama unavyojua malengo ya klabu ni kuchukua kombe hili. Sasa ili kutimiza lengo letu ni lazima tuonyeshe kwa vitendo uwanjani hasa tunapocheza na timu kubwa. Simba ilikuwa ni kipimo kizuri kwetu na tumefanyia kazi vizuri upungufu wetu.”

Katika michezo mitatu iliyocheza Singida kwenye kundi ‘B’ ilimaliza nafasi ya pili ikiwa na pointi sita baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKU na kuichapa APR ya Rwanda 3-1 kisha kupoteza mechi ya mwisho dhidi ya Simba kwa kufungwa 2-0. Kwa upande wa Azam ilimaliza kinara wa kundi ‘A ikiwa na pointi saba baada ya kushinda michezo miwili, sare moja ikifuatiwa na Mlandege iliyomaliza na pointi tatu ambayo leo inacheza na KVZ katika robo fainali ya kwanza.

MSHINE MPYA SIMBA YAANZA KUJIFUA NA WENZAKE….MATOLA AMFUTA KWENYE MECHI YA KESHO… HAWA HAPA MASTAA WANNE WALIOTEMWA TAIFA STARS KIKOSI CHA MWISHO AFCON 2023…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply