Rais wa klabu ya Yanga Eng. Hersi Said ameweka wazi kuwa uendeshaji wa klabu zamani na sasa umebadilika kwa asilimia kubwa sana kwani zamani mtu alikuwa anatoa pesa yake mfukoni kuisaidia klabu lakini kwasasa mfumo ndio unasaidia klabu kujiendesha.
“Kiuchumi hizi klabu mbili haziwezi kusaidizana, kitu kizuri ni kwamba Simba wapo vizuri kiuchumi, na Yanga pia iko vizuri kiuchumi, hakuna mahali ambapo tunaweza kuazimana”.
“Lazima nikiri kwamba mpira umebadilishwa kwa hatua kubwa sana, zamani kulikuwa na watu wanatoa pesa zao mfukoni tena katika mfumo ambao sio sahihi, wa kiholela kwamba anatakiwa mchezaji asajiliwe, we unatoa tu hela mfukoni unamlipa, sasa hivi hakuna”.
” Sasa hivi tumeweka vitu vingi sana kwenye mfumo ambao ni rasmi, mtu inatakiwa asajiliwe, klabu inatakiwa iwe na bajeti yake, pesa zinapatikana wapi, kwa wadhamini na hizo pesa zinalipwa vipi ni mfumo wa benki tu peke yake, huwezi kutoa pesa yako mfukoni ukalishughulikia jambo la klabu tumetoka huko zamani sana” – Alisema Eng. Hersi.
Eng. Hersi ameeleza sababu ya kufanya mabadiliko ya kiuendeshaji ya klabu hiyo, huku sababu kubwa ikiwa ni kipindi kigumu ilichopitia klabu hiyo baada ya kuondoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wa klabu Ndg. Yusuf Manji.
“Yanga ilipita katika wakati mgumu baada ya kuondoka aliyekuwa mwenyekiti na mdhamini wa klabu Yusuph Manji na hiko ni kipimo tosha cha kwamba tunahitaji mfumo sahihi wa kuendesha hizi klabu”
“Kuendesha klabu ya mpira sio kazi ndogo lazima tumpongeze ,lakini baaada ya kuondoka kwake ndio tunagundua hizi Klabu lazima ziendeshwe kwa mfumo ili mtu mmoja asipokuwepo tuweze kuendelea kama Klabu” – Aliongeza Eng. Hersi.
Safi up