Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA AFCON 2023 KUANZA…TANZANIA WAPEWA MBINU ZA KUBEBA KOMBE….

SAA CHACHE KABLA YA AFCON 2023 KUANZA…TANZANIA WAPEWA MBINU ZA KUBEBA KOMBE….

Taifa Stars leo

Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya kuanza kwa Fainali za Mataifa ya Bara la Afrika ‘AFCON 2023’ zitakazofanyikia nchini Ivory Coast, mastaa wa timu ya taifa, Taifa Stars wamepewa ujanja kuhakikisha wanafanya vizuri na kuandika historia kwenye michuano hiyo.

Stars iliyopo Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na DR Congo itacheza mchezo wa kwanza Januari 17 dhidi ya Morocco, ikiwa ni siku nne tangu fainali hizo zitakapoanza rasmi keshokutwa Jumamosi (Januari 13), kisha itavaana na Zambia Januari 21 na kumalizana na DR Congo Januari 24.

Katika kuhakikisha hairudii makosa ya mwaka 2019, ilipocheza Fainali kama hizo na kuaga bila pointi, kocha mkongwe nchini, Salum Suleman Salum aliyewahi kuinoa Malindi ya Zanzibar na klabu mbalimbali za Oman ikiwamo Al-Hamra na Al-Nahdha, amesema kwa jinsi alivyoitazama timu hiyo katika michezo ya kirafiki anaamini vitu vichache vikizingatiwa itafanya vizuri.

Salum ambaye kwa sasa ni kocha wa kituo cha All Star kilichopo Zanzibar, amesema licha ya kupangwa kundi moja na timu kubwa Afrika lakini Stars inapaşwa kucheza mechi zake kwa kujiamini bila hofu, kwani ikikomaa inaweza kupenya kundini au kutoka angalau pointi kwani uwezo inayo.

Kocha huyo aliyeanza kufundisha soka mnwaka 1982 katika timu ya Shangani ya Zanzibar, amesema hadi sasa anamkubali, kocha mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche akiamini kama atazingatiwa na kuungwa mkono basi ataisaidia timu hiyo na kutoa ushindani kwenye fainali hizo.

“Mtazamo wangu tuwe makini katika kubadilisha wachezaji wa akiba, hadi sasa Amrouche yupo sawa na ana uwezo wa kufanya maajabu, cha kuzingatia zaidi ni kwa wachezaji wakipata npira wakimbilie katika box la mpinzani na wacheze pembeni sana mipira,” amesema Salum na kuongeza;

“Nimewatazama kwenye mechi mbalimbali mpaka sasa tunacheza vizuri pia ukiangalia kundi tulilopo nawashauri timu yangu ya Stars kucheza bila ya hofu na wajiamini, pia mashabiki wawe na uzalendo waweke utaifa kwanza.

Licha ya kuweka makazi yake Oman, kocha Salum amesema yuko tayari kufanya kazi nchini.

SOMA NA HII  MAN CITY WAZIDI KUKIWASHA EPL....'JINI LA MAGOLI' HAALAND AZIDI KUTETEMA KAMA MAYELE...