Habari za Simba leo
Habari za michezo

KIUNGO WA KAZI ATEMANA NA SIMBA MAZIMA….AANIKA ANAPOENDA KUKIPIGA ….

admin January 14, 2024 7:47 am

KIRAKA wa zamani wa Simba, Nassoro Kapama amemalizana na waajili wake hao na kuwashukuru mashabiki kwa msimu mmoja na nusu waliokuwa pamoja huku akiweka wazi kuwa ana ofa mbili zinampasua kichwa.

Kapama kupitia akaunti yake ya Instagram ameweka picha aliyovaa jezi ya Simba na kuandika ‘Asanteni hadi wakati mwingine’ hii ni baada ya kuachana na timu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti Kapama amesema; “Nafikiri naweza kwenda Mtibwa Sugar au Geita Gold kwasababu katika ofa nilizokuwa nazo timu hizo mbili zimeweka dau kubwa mezani wakitaka huduma yangu ndani ya miezi sita iliyobaki kumaliza msimu;

“Siwezi kuweka wazi ni adau gani lakini nimefanya mazungumzo na timu zaidi ya tano ila hizo mbili ndio zinanipasua kichwa kabla ya dirisha kufungwa nitakuwa nimefanya uamuzi sahihi,” alisema Kapama

Mbali na timu hizo mbili nyingine ni Namungo FC, JKT Tanzania, Ihefu FC na Mashujaa lakini kwa mujibu wa mchezaji huyo amekiri kuwa ofa nzuri zaidi hadi sasa ni Mtibwa Sugar na Geita Gold.

SIKU MOJA KABLA USAJILI KUFUNGWA…GAMONDI KATAKA MASHINE HII YA KAZI ITUE YANGA…. HUU HAPA UTAJIRI WA MASHINDANO YA AFCON….TIMU ZA TAIFA KULAMBA MAMILIONI YA PESA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply